Mpango wa usimamizi wa Kaunti ya King 2024
Mpango wa usimamizi wa Kaunti ya King 2024
Mafuriko yametokea King County. Hatari za mafuriko zinadhibitiwa kupitia Mpango wa Kudhibiti Mafuriko wa King County. Kamilisha utafiti ili kutoa mawazo yako kuhusu namna ya kujenga mustakabali ulio dhabiti dhidi ya mafuriko. Unaweza pia kutumia tovuti hii kusoma zaidi kuhusu mafuriko katika Kaunti ya King na rasilimali zilizopo kupunguza hatari za mafuriko.
Huduma za ukalimani na utafsiri zinapatikana bila gharama kwako. Ikiwa unazihitaji, tafadhali wasiliana nasi kupitia 206-263-2677. English | Español | Tiếng Việt | Soomaali | 한국어 | Русский язык 繁體中文 | Kiswahili | Français | Mandi'nka kango | ខ្មែរ |
|
Community flood planning survey
You don’t need to be an expert in flooding to provide valuable input. Your responses to the following questions will help shape the priorities in the next flood plan. This survey will...
Tupange pamoja kustahimili mafuriko
Mafuriko ni maafa ya asili ya kawaida katika eneo letu na ni sehemu ya maisha katika Kaunti ya King. Mafuriko yanaweza kuharibu vitongoji. Mafuriko huharibu nyumba, kuharibu mali ya kibinafsi na kuweka maisha hatarini. Mafuriko pia huathiri ufikiaji wa kazi, maduka na shule na yanaweza kuharibu maeneo ya wazi ya jamii. Mafuriko yanaweza kutokea mara kwa mara na makubwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Majanga ya asili huathiri watu kwa njia tofauti, huku wengine wakiwa na wakati mgumu wa kupona, au pengine kutopona kabisa. Kujenga uwezo wa kustahimili mafuriko kunamaanisha kuwa tunaongeza uwezo wa watu na jamii kupata nafuu haraka kutokana na athari zozote zinazoletwa na mafuriko kwenye milango yetu. Mafuriko hayatatoweka katika King County, lakini kuwa tayari kunaweza kupunguza hatari kwa jamii, familia na watu binafsi.
Mpango wa mafuriko huelekeza jinsi tunavyodhibiti hatari za mafuriko na jinsi manufaa ya juhudi zetu yanavyosambazwa katika kaunti nzima. Taarifa kwenye tovuti hii imepangwa katika sehemu tano:
- Mafuriko na kujenga uwezo wa kustahamili mafuriko – habari ya usuli na nyenzo
- Kupanga utangulizi wa kustahamili mafuriko katika mpango, mchakato wa kusasisha mpango, na kwa nini mpango huo ni muhimu.
- Shiriki mawazo yako – maswali ya uchunguzi ili kufahamisha upeo na vitendo vilivyoainishwa katika mpango
- Mikutano na matukio – kumbi za kujifunza kuhusu mafuriko na kushiriki maarifa ya eneo lako
- Tulichosikia kutoka kwako – ripoti kuhusu maoni ambayo tumepokea hadi sasa
Jisajili kupokea sasisho za barua pepe kuhusu mpango wa mafuriko!
Mafuriko yam to Snoqualmie karibu na Duvall mnamo desemba 2015.
Anwani
Kwa maelezo ya jumla au usaidizi wa maswali kuhusu mafuriko, tafadhali wasiliana na:
Mto wa Kaunti ya King na sehemu ya usimamizi wa mafuriko
206-477-4812
Kwa maswali kuhusu sasisho la mpango wa mafuriko, tafadhali wasiliana na:
Meneja mradi
206-477-4786
Jason.Wilkinson@kingcounty.gov
Kwa maswali kuhusu fursa za ushiriki wa jamii ya mpango wa mafuriko au jinsi ya kuwasilisha maoni, tafadhali wasiliana na:
Mratibu wa ushirikiano wa jamii wa mpango wa mafuriko
206-263-2677